logo

NOW ON AIR

Listen in Live

UAE yazuia utoaji wa visa kwa Wakenya kwa sababu ya Covid 19

Hata hivyo ni Pakistan pekee iliyothibitisha habari hizo ikiwanukuu maafisa wa serikali

image
na Radio Jambo

Yanayojiri20 November 2020 - 09:43

Muhtasari


 

  •  Hata hivyo ni Pakistan pekee iliyothibitisha habari hizo ikiwanukuu maafisa wa serikali
  •  Kwa  sasa watu 1300 wamefariki kwa ajili ya ugonjwa huo huku Zaidi ya 70,500 wakiambukizwa .Mapema mwezi huu serikali ililazimika kupiga marufuku mikutano ya kisiasa  ili kuzuia  ongezeko la visa vya maambukizi

 Muungano wa Milki za kiaranu UAE  umefutilia mbali utoaji wa visa kwa wakenya wanaozuru taifa hilo  na wageni kutoka nchi nyingine 11

 Mataifa mengine yaliathiriwa na hatua hiyo ya UAE ni  Pakistan, Iran, Yemen, Syria, Somalia, Iraq, Turkey, Afghanistan, Syria  na  Libya.

 Hata hivyo ni Pakistan pekee iliyothibitisha habari hizo ikiwanukuu maafisa wa serikali .

Wizara ya mashauri ya kigeni ya Pakistan  imesema  marfuku hiyo haitawaathiri walio na visa tayari .

 Haijabainika ni vitengo vipi vya visa ambavyo vimeathiriwa na hatua hiyo ya UAE .Kenya ilivunja  rekodi ya maambukizi ya kila siku baaa ya visa Zaidi ya 1500 kuanza kuripotiwa  huku idadi ya wanaofariki pia ikipanda .

 Kwa  sasa watu 1300 wamefariki kwa ajili ya ugonjwa huo huku Zaidi ya 70,500 wakiambukizwa .Mapema mwezi huu serikali ililazimika kupiga marufuku mikutano ya kisiasa  ili kuzuia  ongezeko la visa vya maambukizi

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved