- Madaktari waliwaita polisi wa Kilimani kumkamata mshukiwa alipokwenda kuwatembelea hospitalini
- Mshukiwa amekanusha mashtaka yote dhidi yake
Baba mmoja wa kambo ameshtakiwa kwa kuwadhulumu kimapenzi bintiye mwenye umri wa miaka minne na mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu.
Mshukiwa alifikishwa mbele ya hakimu mkuu wa Makadara siku ya ijumaa .Anashtumiwa kwa kutekeleza kosa hilo tarehe 16 mwezi huu Kibra ,Makina .
Katika kosa la pili mshukiwa anashtumiwa kwa kumdhulumu kimapenzi mtoto wa siku nne siku iyo hiyo .katika mashtaka yote mawili mshukiwa amekabiliwa na kosa mbadala la kuwafanyoa watoto vitendo visivyofaa .
Kulingana na stakabadhi za mahakama , tukio hilo lilifanyika wakati mama ya watoto hao alipowaacha na mshukiwa ili kwenda msalani .
Aliporejea mwanamke huyo aligundua kwamba wanawe walikuwa wakipitia uchungu . mtoto wake wa kiume alikuwa amefura mdomo na kupata matatizo kuketi chini ilhali mtoto wa kike alikuwa na majeraha katika sehemu zake za siri .
Mume wake alikanusha kuwasababishia majeraha watoto hao . Baadaye mwanamke huyo aliwapeleka watoto hao hospitalini ambapo ilithibitishwa kwamba walikuwa wamedhulumiwa kingono .
Mshukiwa alikamatwa novemba tarehe 17 alipokwenda hospitalini kuwatembelea waathiriwa .madaktari waliwaarifu polisi wa kituo cha Kilimani waliokuja na kumkamata mshukiwa .
Amekanusha mashtaka dhidi yake na upande wa mashtaka umetaka kumzuilia kwa muda zaidi
Hakimu mkuu Heston Nyaga ameagiza mshukiwa kuzuiliwa hadi jumatano wiki ijayo kwa maelezo zaidi