- Mshukiwa alikuwa akiishi mashambani baada ya kutofautiana na mume wake
- Alimwagia maji kabla ya kumsakama hadi kumwuua
Makachero wa DCI siku ya ijumaa wameruhusiwa kumzuilia kwa siku 14 mwanamke anayeshtumiwa kwa kumuua mke mwenza kwa kumwagia maji na kisha kumnyonga hadi kumuua .
Jescah Kalumu Mungatu anashukiwa kumuua kwa kumnyonga Abbisseneh Katungu baada ya kumwagia maji moto usiku ya tarehe 14 mwezi huu katika mtaa wa makadara ,Nairobi
Kwa mujibu wa stakabadhi zilizowasilishwa kortini kisa hicho kilitokea baada ya wanawake hao wawili kugombana wakati mume wao hakuwa nyumbani .
Hakimu mkuu wa makadra Heston Nyaga alikubali ombi la DCI kusalia na mshukiwa ili kuruhusu uchunguzi kuendelea
DCI imesema tukio hilo liliripotiwa katika kituo cha polisi cha Lunga lunga na mwenyekiti wa mta wa mabanda wa Sinai Kioko Musau mwendo wa saa mbili usiku .
Ripoti ya polisi imesema ,Mungatu ambaye ni mke wa kwanza alikuwa akiishi mashambani baad ya kutofautiana na mume wake .ni wakai alipokuwa nyumani ndipo mume wake alimuoa Katungu kama mke wa pili . Baada ya mke wa kwanza kugundua kilichofanyika alifunga safari kuja Nairobi .
Afisa nayechunguza kesi hiyo anasema wanahitaji muda Zaidi kumpeleska mshukiwa kwa ukaguzi wa akili . Amesema pindi uchunguzi utakapokamilishwa wataipeleka faili yake kwa DPP kwa maelekezo na ushauri .suala hilo litatajwa Disemba tarehe 2