Watoto wanafanya uhalifu

Fuatilieni shughuli za watoto wenu wakiwa nyumbani na mitandaoni ,DCI yaonya

Wasichana hao saba walitoweka wiki jana

Muhtasari
  •  Mkuu Wa DCI  George Kinoti  amesema wanalisaka genge la wahalifu ambalo linawatumia watoto kufanya vitendo visivyo halali
  •  DCI  imewaokoa wasichana sita walioripotiwa kupotea  baada ya video kusambazwa mitandaoni kutaka maelezo yatakayosaidia warejee nyumbani

 

Mkuu wa DCI George Kinoti

 Idara ya DCI imewashauri wazazi  kuwa waangalifu kuhusu mienendo ya watoto wao wakiwa nyumbani na wanachofanya mitandaoni

 Mkuu Wa DCI  George Kinoti  amesema wanalisaka genge la wahalifu ambalo linawatumia watoto kufanya vitendo visivyo halali

Kinoti  amewaonya wazazi kwamba wanafaa kufuatilia shughuli za wanao mitandaoni pia

" Uchunguzi ukiendelea tungependa pia kuwaonya watu wanaowatumia watoto kutekeleza uhalifu na kujihusisha na vitendo vingine vibaya kupitia mitandao ya kijamii’ amesema Kinoti

 Makachero wanalichunguza kundi moja linalotumia mitandao ya kijamii kuwatumia waichana wa shule kujihusisha na  uhalifu kama vile kuteneza picha za  ponografia na kuwafanya watoto hao kutoweka kutoka majumbani kwa siku kadhaa .

 DCI  imewaokoa wasichana sita walioripotiwa kupotea  baada ya video kusambazwa mitandaoni kutaka maelezo yatakayosaidia warejee nyumbani .

 Kulingana na mwanamke mmoja aliyetengeza ombi hilo kupitia njia ya video  wasichanahao walitoweka tarehe 14 Novemba  baada ya kuhadiwa kutoka makwao na mtu aliyejulikana  .wasichana hao saba walikuwa na umri wa miaka 16 kutoka mtaa wa Komarock ,Nairobi