- Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema visa hivyo ni kutoka sampuli 7,387 zilizopimwa
- Wagonjwa 31 wapo ICU .Watu 265 wamepona ugonjwa huo na kufikisha 52,974 watu waliopona ugonjwa huo hadi kufikia sasa .
Kenya siku ya jumatano imesajili visa vipya 810 vya corona na kufikisha 79,322 jumla ya idadi ya visa hivyo nchini .
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema visa hivyo ni kutoka sampuli 7,387 zilizopimwa katika saa 24 zilziopita na sasa idadi ya jumla ya sampuli zilziopimwa ni 855,403 . idadi ya watu waliofariki kwa ajili ya Corona imeongezeka hadi 1,417 baada ya watu wanane zaidi kuaga dunia .
Kagwe amesema kwa sasa kuna wagonjwa 1,198 waliolazwa katika hospitali mbali mbali nchini huku watu 7,169 wakiwa chini ya mpango wa kutunzwa nyumbani .
Wagonjwa 31 wapo ICU .Watu 265 wamepona ugonjwa huo na kufikisha 52,974 watu waliopona ugonjwa huo hadi kufikia sasa .
Katika visa vipya vilivyoripotiwa 792 ni wakenya ilhali 18 ni raia wa kigeni ,mgonjwa wa umri wa chini ana mwaka mmoja ilhali wa umri wa juu ana miaka 87 . watu 475 ni wanaume ilhali 335 ni wanawake