BBI

Raila: Mapendekezo ya BBI yanalenga kuboresha utawala wa Kenya

Sahihi zitaanza kukusanya leo kwa siku 7

Muhtasari
  •  Odinga amesema masuala mengi yanaweza kushughulikiwa kupitia sheria na sera za serikali 
  •  Odinga amewahimiza wakenya kujitokeza na kuweka saini zao ili kufanikisha kura ya maoni 

 

Kiongozi wa ODM Raila Odinga

 Kiongozi wa ODM Raila  Odinga  amesema kwamba  wajibu wa mchakato wa BBI ni kuimarisha utawala wa Kenya .

Raila Odinga  amesema  masuala yanayohusu wananchi na hali ya uchumi yanaweza kushughulikiwa kupitia sheria na sera za serikali . Alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa  ukusanyaji wa sahihi za BBI katika ukumbi wa KICC .

 Kuhusu wadhifa ya msimamizi wa idara ya mahakama ambalo limekuwa donda sugu katika ripoti ya BBI   Raila amesema  jopo la uteuzi litampa rais majina ya watu watatu ambao yatatumwa bungeni kupigwa msasa na kisha moja kuteuliwa na rais .

" Hilo litavuruga vipi  uhuru wa  idara ya mahakama? Raila amesema

" Tumepitia mengi ya uhasama na  siku ngumu  na hata vipindi vya kubaguliwa na tunaweza kuona tunakotaka kwenda’

 Amewahimiza wakenya kujitokeza kwa wingi na kutia saini  zinazohitajika kufanikisha kura ya maoni ili kuirekebisha katiba .