Huko na ni matusi tu!

Uhuru:Heri nilale kuliko kuingia Twitter

Uhuru azungumza kuhusu kukataa kutumia twitter

Muhtasari

 

  •  Rais amesema anapendelea kukutana ana kwa ana na viongozi kwa majadiliano badala ya kutegemea twitter 
  •  Rais kenyatta alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la kukusanya sahihi za BBI 

 

 

Rais Uhuru Kenyatta

 Rais Uhuru kenyatta alizua  kicheko siku ya jumatano aliposema mbona hataki kuingia twitter na  mitandao ya kijamii . Rais ambaye alikuwa akieleza kuhusu mikutano ambayo  amekuwa akifanya na viongozi   mbali mbali ili kusikiliza kuhusu mapendekezo yao  kuhusu BBI rais alisema  hategemi Twitter kupata maelezo na mapendekezo ya  wengine . Rais  amesema ;

 ‘Mimi sipendi kwa magazeti ,mimi nakutana na watu tu ….kwa sababu mimi sio mtu  wa hiyo . Hata twitter niliondoka …hii kitu ni bure…! ni matusi tu .. hakuna kitu inaendelea .unakaa hapo unasoma hulali ….unasomaaa …huyu ..unapiga simu unaona vile huyu mtu amenitusi ..afadhali nilalale bwana .. niongee…nipige story na mama hapo  kidogo hapo ..nilale niamke ..niende kazi ..dunia iendelee …’

 Kumekuwa na ongezeko la matumizi ya mitandao  ya kijamii na hasa twitter kueleza misimamo mbali mbali ya kisiasa huku naibu rais William Ruto akiwa miongoni mwa viongozi wanaotumia sana twitter .

 Ruto amekuwa akitumia sana twitter kupaza sauti yake kuhusu masuala mbali mbali lakini yaonekana mkuu wake hapendi mbinu hiyo ya mawasiliano .

Rais alikuwa akizungumza siku ya jumatano wakati wa uzinduzi wa  ukusanyaji wa sahihi za kufanikisha kura ya maoni kupitia BBI . Amesema  mapendekezo ambayo yametolewa na wakenya mbali mbali yatazingatiwa lakini wananchi wanafaa kufahamu kwamba katiba inaweza kurekebishwa kwa awamu kulingana na mahitaji ya wakati uliopo