Mama akata nyeti za mwanawe Kiambu

Uhalifu
Uhalifu

Mtoto wa kiume mwenye umri mwaka mmoja anapigania maisha yake katika hospitali ya Kijabe baada ya mamake kumkata nyeti zake.

Polisi wameanzisha msako kumtafuta mama huyo ambaye alikwenda mafichoni punde tu baada ya kudaiwa kutekeleza uovu huo.

Afisa  mkuu wa polisi katika eneo la Tigoni, kaunti ya Kiambu Mwaniki Ireri alitbitisha kisa hicho na kusema kwamba kilitokea katika Kijiji cha Kamandura mapema siku ya Jumatano.

 

Ireri alisema mtoto huyo amelazwa na hali yake bado ni mbaya.

Bado haijabainika haswa nini kilimchochea mama huyo wa watoto wawili kumdhulumu mwanawe kiasi hicho.

Kulingana na majirani, babake mtoto huyo alitaka kujua kwanini mwanawe alikuwa akilia na mamake hashughuliki. Alipouliza mamake alidai kwamba mvulana huyo alikuwa ameanguka na kuumia mguu akicheza.

Babake alipomkagua mwanawe hakuona jeraha lolote kwa mguu na kushtuka alimpo mvua nguo na kugundua kwamba alikuwa amenyofolewa. Alimkimbiza hospitalini na msako dhidi mamake ukaanza.

Kwingineko,

Polisi katika eneo la Shinyalu kaunti ya Kakamega wamemkamata mwanamume wa miaka 60 kuhusiana na kifo cha mkewe.

Inadaiwa kwamba mshukiwa alimpiga mkewe na kumjeruhi vibaya hali iliyopelekea kifo chake.

 

Wawili hao ambao walikuwa waraibu wa pombe wanadaiwa kuzozania shilingi mia sita za kununua chang’aa.