Maseneta wataanza kusikiza kesi ya kufurushwa kwa gavana wa Nairobi Mike Sonko siku ya jumatano .
Spika wa senate Ken Lusaka ameyasema hayo kupitia arifa ya gazeti rasmi la serikali .
Kikao hicho kitafanyika katika majengo ya bunge kuanzia saa tatu asubuhi .
Sonko alifurushwa na wakilishi wa kaunti katika hali ya kutatanisha baada ya viongozi 88 kupiga kura ya kutokuwa na imani naye .