'Tuko tayari kupigana na vyama vingine katika kinyanganyiro cha Urais' Chama cha NRA chaapa

Muhtasari
  • Chama cha NRA chaapa kupigana na vyama vingine vya kisiasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022

Chama kipya cha kisiasa cha National Reconstruction Alliance kimeahidi kuonyesha vyama vingine kivumbi mwaka wa 2022.

Chama hicho kilichosajiliwa hivi majuzi na Wakili Riziki Dunstan na wenzake Amemba Magufuli na Fred Ojiambo tayari kina memba 500,000.

Chama hicho ambacho kitazinduliwa rasmi mwezi Machi ama April kwa sababu ya corona, kimewaomba vijana kujiandaa kupiga kura mwaka wa 2022.

 

Katika ujumbe wake kwa wanahabari msimamizi wa vijana Kisii Joshua Nyabanayo ameomba vijana kujitayarisha kwa shughuli hii kwa kuchukua vitambulisho na kadi za kupiga kura.

Vile vile Lumala Lumala ambaye ni msimamizi wa wanafunzi katika chuo kikuu cha Masinde Muliro amesemaViongozi wa vyama vikongwe watakiona Cha mtema kuni mwaka wa 2022.

"Kama chama tuko tayari kupigana na vyama vikuu hapa Kenya.Wanafaa wawe tayari kupigana Vita,ngumu zaidi maishani mwao."