Somalia inafaa kukoma kuiingiza Kenya katika masuala yake ya ndani ,msemaji wa serikali ya Cyrus Oguna amesema .
Akiwahutubia wandishi a Habari siku ya alhamisi Oguna amesema Kenya haitakubali kuingizwa katika siasa za ndani ya Somalia . Oguna amesema matukio yanayoshuhudiwa katika kaunti ya Mandera yana chimbuko lake katika mchakati wa kisiasa nchini Somalia .
" Makabiliano kati ya makundi hayo hayasababishi tu hofu miongoni mwa watu wetu katika mpaka huo lakini pia yanasababisha watu kuhama makao yao katika eneo la Gedo nchini Somalia’ amesema Oguna .
Pia alikana madai kwamba majeshi ya Kenya nchini Somalia yanajihusisha na biashara haramu ya makaa na sukari .
Aliwahimiza viongozi wa Somalia kuunda mazingira mazuri ili kufanikisha mazungumzo ya kumaliza migogoro kati ao ambayo kwa muda mrefu imeikosehsa nchi hiyo Amani’ amesema Oguna
" Madai ya Somalia kwamba Kenya inafadhili makundi ya wapiganaji ili kuleata sumbufu nchini humo hayana msingi wowote’ .
Oguna amesema wakenya wanatambulika kwa ukarimu wao .
" kwa sababu ya hilo wasomli wengi wanakimbilia hapa panapotokea machafuko nchini mwao .Bado wanavuka mpaka kuingia Kenya kutafuta baadhi ya huduma’ amesema
‘ Kwa hivyo haitakuwa bora kwa Kenya kutaka kusababisha hali ya msukosuko nchini Somalia kwa watu ambao Kenya ndio huwapa hifadhi’.