Nidhamu ya trafiki

Kikosi chaundwa kukabiliana na polisi ‘watundu wa Trafiki’

Mutyambai aliagiza vizuizi kuwekwa tu kupitia idhini ya makamanda wa maeneo na pasiwe na Zaidi ya polisi 10 katika majukumu ya kusimamia vituo hivyo .

Muhtasari
 •  Vizuizi vya barabarani vinafaa kuwekwa baada ya idhini kutolewa na  makanda wa maeneo wa vikosi katika  maeneo  .
 •  Amewaonya makanda wa wadi na kaunti  ndogo ambako vizuizi hivyo vitapatikana watachukuliwa hatua na kuhamishwa .
Polisi wa trafiki

Makao makuu ya polisi yametuma vikosi maalum  vya maafisa wa kukabiliana na polisi wa trafiki watundi ambao wameendelea kuweka vizuizi vya kudumu barabarani .

 Hi ni  licha ya inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai kuagiza kwamba vizuizi vya kudumu viondolewe katika barabara kuu na badala  vitumie vizuizi vya muda  .

 Kwa mfano katika eneo la Rift Valley  ambako kuna barabara kubwa inayounganisha  Kenya-Uganda-Tanzania-Rwanda -Sudan Kusini-DR Congo  maafisa wa trafiki wangali wanatumia vizuizi vya barabarani licha ya kukatazwa kufanya hivyo .

 Kamanda wa polisi wa eneo hilo Marcus Ocholla  amesema aligundua ongezko la vizuzi vya muda vinavyowekwa na polisi ili kujinufaisha kibinafasi  na sio kuwakabili wanaokiuka sheria za trafiki .

 Vizuizi vya barabarani vinafaa kuwekwa baada ya idhini kutolewa na  makanda wa maeneo wa vikosi katika  maeneo  .

 Amewaonya makanda wa wadi na kaunti  ndogo ambako vizuizi hivyo vitapatikana watachukuliwa hatua na kuhamishwa .

 Hatua hiyo ni ya hivi punde ya usimamizi wa polisi kukabiliana na polisi wakaidi wa trafiki ambao wameunda mseto mbadala wa sheria za kutekelezwa  barabarani .

 Mutyambai   aliagiza vizuizi kuwekwa tu kupitia idhini ya makamanda wa maeneo na pasiwe na Zaidi ya polisi 10 katika majukumu ya kusimamia vituo hivyo .

 Alifichua kwamba makamanda watawajibikia maovu yanayotekelezwa na polisi katika maeneo yao ambao wamepewa jukumu la kusimamia vizuizi hivyo vinavyofaa kuwekwa katika maeneo Fulani pekee kwenye barabara kuu za humu nchini .Baadhi ya njia  hizo  ni ;

 1. Mombasa-Malindi
 2. Mobasa-Lungalunga
 3. Mombasa-Mackinon
 4. Mackinon-Voi-Mwatate-Taveta
 5. Voi-Mtito Andei
 6. Mtito Andei-Sultan Hamud
 7. Sultan Hamud-Machakos Kyunvi Junction
 8. Thika-Mwingi
 9. Athi River-Kajiado-Namanga
 10. Nairobi-Thika-Muranga
 11. Ruiru-Kiambu-Limuru
 12. Muranga-Nyeri
 13. Nyeri-Nanyuki
 14. Nyeri-Nyahururu-Nakuru
 15. Mwea-Embu
 16. Meru-Isiolo-Nanyuki
 17. Garisa-Mwingi
 18. Nairobi-Kinungi
 19. Kinungi-Nakuru
 20. Nakuru-Mlango Nne
 21. Mlango Nne-Eldoret
 22. Eldoret-Kitale-Kapenguria
 23. Maimahiu-Narok
 24. Narok-Bomet
 25. Bomet-Kisii
 26. Homabay-Kisumu
 27. Kisumu-Busia
 28. Busia-Malaba-Bungoma
 29. Mau Summit-Kerocho-Kisumu
 30. Webuye-Kakamega-Kisumu.