Sonko Mashakani

Sonko mashakani baada ya polisi kuwakamata wasaidizi wake na kufanya misako majumbani mwao

Hakimu aliagiza wazuiliwe hadi siku ya jumatatu wakati watakapofikishwa kortini pamoja na Sonko kusikiza ombi la kuwazuilia kwa siku 30 .

Muhtasari
  •  Oparesheni hiyo ilifanywa na polisi kutoka kitengo cha kukabiliana na ugaidi .
  •  Baadhi ya  watu wa kwanza kukamatwa  wiki jana ni  wasaidizi wa Sonko Clifford Ouko  na Benjamin Ochieng.
Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko

 Polisi wamezidisha  kampeini yao dhidi ya gavana wa zamani   wa  Nairobi Mike Sonko  kwa kuwakamata wasaidizi wake,kufanya misako majumbani mwao na kusababisha hofu  kuhusu madai ya ugaidi dhidi ya gavana huyo wa zamani .

 Wasaidizi wake saba Zaidi walikamatwa siku za ijumaa na jumamosi  na polisi waliokuwa wamevalia sare za raia .  Baadhi ya wasaidizi hao walikuwa nje ya  City Hall ilhali wengine walikuwa majumbani mwao . Wengi wa wasaidizi wa   Sonko walipatwa na hofo ya kukamatwa kufuatia msururu wa kamata kamata hizo .

 Hatua hiyo imezidisha hadi watu tisa akiwemo Sonko waliokamatwa kuhusiana nan a madai kwamba gavana huyo anasadia kuunda kundi la wapiganaji kutekeleza mashambulizi nchini .

 Oparesheni hiyo ilifanywa na polisi kutoka kitengo cha kukabiliana na ugaidi .

 Baadhi ya  watu wa kwanza kukamatwa  wiki jana ni  wasaidizi wa Sonko Clifford Ouko  na Benjamin Ochieng.  Siku  ya alhamisi  waliwasilishwa katika  mahakama  ya kahawa west , gereza la kamiti ili kujibu mashtaka ya kujaribu kumuokoa Sonko kutoka seli .

 Upande wa mashtaka unataka wazuiliwe kwa siku 30 ili wakamailishe uchunguzi .  Hakimu aliagiza wazuiliwe hadi siku ya jumatatu  wakati  watakapofikishwa kortini pamoja na Sonko  kusikiza ombi la kuwazuilia kwa siku 30 .