Mahakama siku ya jumanne itatathmini ripoti za matibabu za gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko na kuamua Iwapo anafaa kurejeshwa seli au hospitalini .
Mmoja wa mawakili wake Evans Ondieki amesema hospitali ya Nairobi iliwasilisha ripoti hiyo kama ilivyoagizwa na mahakama .Suala hilo litashughulikiwa na mahakama ya Kahawa west tarehe 16 Februari .
“ Presha yake ya damu iko juu na hospitali imewasilisha ripoti yake kwa mahakama kabla ya uamuzi kufanywa siku ya jumanne .Ni baada ya hapo ambapo itaamuliwa Iwapo anafaa kuzuiliwa na polisi ama hospitalini’ amesema Ondieki
Hakimu wa Kahawa West aliagiza kwamba Sonko Sonkoo apelekwe hospitalini na ripoti itolewe kuhusu hali yake ya afya . Takriban maafisa 9 wa polisi wanamlinda hospitalini ambako amelazwa tangu jumatatu usiku .