Sonko

Sonko atakuwa hospitalini siku ya Valentine’s kabla ya korti kutoa uamuzi

Takriban maafisa 9 wa polisi wanamlinda hospitalini ambako amelazwa tangu jumatatu usiku .

Muhtasari
  •  Mmoja wa mawakili wake Evans Ondieki amesema hospitali ya Nairobi iliwasilisha ripoti hiyo kama ilivyoagizwa na mahakama .
  • Suala hilo litashughulikiwa na mahakama ya Kahawa west   tarehe 16 Februari .
Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko

 Mahakama siku ya jumanne itatathmini ripoti za matibabu za gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko na kuamua Iwapo anafaa kurejeshwa seli au hospitalini .

 Mmoja wa mawakili wake Evans Ondieki amesema hospitali ya Nairobi iliwasilisha ripoti hiyo kama ilivyoagizwa na mahakama .Suala hilo litashughulikiwa na mahakama ya Kahawa west   tarehe 16 Februari .

 “ Presha yake ya damu iko juu  na hospitali imewasilisha ripoti yake kwa mahakama kabla ya uamuzi kufanywa siku ya jumanne .Ni baada ya hapo ambapo itaamuliwa Iwapo anafaa kuzuiliwa na polisi ama hospitalini’ amesema Ondieki

 Hakimu wa  Kahawa West aliagiza kwamba Sonko  Sonkoo apelekwe hospitalini  na ripoti itolewe  kuhusu hali yake ya afya . Takriban maafisa 9 wa polisi wanamlinda  hospitalini  ambako amelazwa tangu  jumatatu usiku .