Covid 19

75 wapatikana na Corona huku 56 wakipona

Kuna wagonjwa 347 waliolazwa hospitalini kote nchini huku 1,275 wakiwa chini ya mpango wa kutunzwa nyumbani .Wagonjwa 33 wapo ICU

Muhtasari
  • Jumla ya sampuli zilizopimwa sasa ni 1,241,368  .Kutoka visa  hivyo 62 I wakenya ilhali 13 ni raia wa kigeni .
  • Wanaumeni 48 ilhali wanawake ni 27 .Mgonjwa wa umri wa chini  ni mtoto wa miaka 5 ilhali wa umri wa juu ana miaka 89 .
Picha: REUTERS
Picha: REUTERS

Watu 75 wamepatikana na virusi vya Corona baada ya sampuli 3,025 kupimwa katika saa24 zilizopita  na kufikisha visa hivyo kuwa 102,867 .

Jumla ya sampuli zilizopimwa sasa ni 1,241,368  .Kutoka visa  hivyo 62 I wakenya ilhali 13 ni raia wa kigeni .Wanaumeni 48 ilhali wanawake ni 27 .Mgonjwa wa umri wa chini  ni mtoto wa miaka 5 ilhali wa umri wa juu ana miaka 89 .

Visa vya Corona katika kila kaunti
Image: Yusuf Juma
 

Leo watu 56 wamepona ugonjwa huo  na kufikisha 85,008 idadi ya waliopona Corona hadi sasa .Hakuna maafa yaliyoripotiwa leo na idadi hiyo inasalia kuwa  1,795 . Kuna wagonjwa 347 waliolazwa hospitalini kote  nchini huku 1,275 wakiwa chini ya mpango wa kutunzwa nyumbani .Wagonjwa 33 wapo ICU