Covid-19: Watu 10 wapoteza maisha yao kutokana na corona

Muhtasari
  • Watu 194 wapatikana na corona huku 55 wakiwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi ICU
  • Pia 39 wamepona maradhi hayo huku 10 wakipoteza maisha yao kutokana na corona
Picha: REUTERS
Picha: REUTERS

Visa 194 vya corona vimeripotiwa nchini siku ya Jumanne baada ya sampuli 3,935 kupimwa katika saa 24 zilizopita .

Idadi hiyo inafikisha 104,500 jumla ya visa hivyo hadi sasa huku sampuli zilizopimwa zikifika 1,273,281.

Kutoka visa hivyo 146 ni wakenya ilhali raia wa kigeni ni 48. mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 6 ilhali wa umri wa juu ana miaka 95

 

Wagonjwa 108 ni wanaume huku 86 wakiwa wanawake, kulingana na kaunti, kaunti ya Nairobi imeongoza kwa visa 132 vipya vya maabukizi ya corona ikifuatwa na kaunti ya Kiambu na visa 9

Wagonjwa 39 wamepona ugonjwa huo huku idadi hiyo ikifika 85,665  Watu 3 wamepona wakipokea matibabu wakiwa nyumbani huku 36 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 10 wamepoteza maisha yao kutokana na maradhi hayo na kufikisha idadi jumla 1,837 ya watu walioga dunia.

Kuna wagonjwa 344 ambao wamelazwa hospitalini ilhali 1,283 wapo chini ya mpango wa utunzi nyumbani .

Wagonjwa 55 wapo katika kitengo cha ICU.