Tiger Woods afanyiwa upasuaji baada ya gari lake kubingiria

Muhtasari

• Idara ya polisi ya jimbo Los Angeles ilisema kwamba "ilishughulikia ajali ya gari moja"  ambalo " liliharibika vibaya "

Mabaki ya gari alimokuwa bingwa wa gofu Tiger Woods
Mabaki ya gari alimokuwa bingwa wa gofu Tiger Woods

Nyota wa gofu duniani Tiger Woods lihusika katika ajali mbaya ya barabarani siku ya Jumanne asubuhi baada ya gari lake kubingiria mara kadohaa.

Woods alifanyiwa upasuaji katika mguu wake uliyovunjika mara kadhaa katika ajali ya gari huko Los Angeles, California.

Idara ya polisi ya jimbo Los Angeles ilisema kwamba "ilishughulikia ajali ya gari moja"  ambalo " liliharibika vibaya ".

Bingwa huyo wa gofu duniani mara 15, mwenye umri wa miaka 45, alilazimika "kutolewa kutoka kwa mabaki ya gari lake" na wazima moto na maafisa utabibu.

 Wakala wa Woods Mark Steinberg alisema: "Kwa sasa yuko kwenye upasuaji na tunawashukuru kwa msaada."

Steinberg alithibitisha kiwango cha majeraha ya Woods "majeraha mengi ya miguu".

Tiger woods major win
Tiger woods major win

Woods alikuwa kwenye Klabu cha Riviera huko LA mwishoni mwa wiki kama mwenyeji wa mashindano ya Mwaliko ya Genesis.

Taarifa kutoka Idara ya polisi ya Los Angeles ilisema kwamba hiyo ilitokea "kwenye mpaka wa Rolling Hills Estates na Rancho Palos Verdes" Jumanne asubuhi saa za Amerika.

Iliongeza: "Bwana Woods aliondolewa kutoka kwa mabaki ya gari lake na wazima moto na wahudumu wa afya waliolazimika kukata mabaki ya gari hilo kumuokoa, kisha akapelekwa hospitali ya eneo hilo na ambulensi." Idara ya Zimamoto ya Kaunti ya LA ilisema:

Woods alihusika katika ajali ya gari mnamo Novemba 2009 ambayo mwishowe ilisababisha kukiri kwa uaminifu na kuvunjika kwa ndoa yake.

Kisha akapumzika kutoka gofu kwa muda na  lakini akarejea baadaye.