Aina mpya ya virusi vya Covid-19 nchini Tanzania yazua hofu

Muhtasari

• Aina mpya ya virusi vya corona nchini Tanzania imejibadilisha zaidi ya mara kumi kuliko aina zingine za SARS-Cov-2.

• Wanasayansi bado hawajui kama aina hiyo ya virusi kutoka Tanzania inaambukizana zaidi kuliko aina zingine.

TAARIFA YA JOHN MUCHANGI 

 

Watafiti wanasema chanjo ya Covid-19 inayotumiwa nchini Kenya ina uwezekano mkubwa kukabiliana na aina mpya ya virusi vya Covid-19 ikiwemo aina mpya ambayo ni hatari kutoka Tanzania.

Aina mpya ya virusi vya corona nchini Tanzania imejibadilisha zaidi ya mara kumi kuliko aina zingine za SARS-Cov-2, kulingana na ripoti iliyowasilishwa kwa Shirika la Afya duniani wiki iliyopita.

Wanasayansi bado hawajui kama aina hiyo ya virusi kutoka Tanzania inaambukizana zaidi kuliko aina zingine.

Watafiti wa Kenya siku ya Jumatano walisema chanjo za sasa za Covid-19 zinaweza kusajili ufanisi dhidi ya aina hiyo mpya.

"Ni asili ya virusi kuendelea kubadilika na haitabiriki sana mwelekeo watakaochukua," alisema Dkt. Njagi Kumantha, mtaalam wa mifumo ya afya baada ya kuchukua chanjo ya AstraZeneca Jumatano.

"Lakini ikiwa umepewa chanjo dhidi ya aina moja, pia itakulinda dhidi ya aina zingine kwa sababu watakabiliwa na athari sawa kwa mwili, kwa sababu ya kinga ya mwili."

Wimbi la tatu la maambukizi ya Covid nchini Kenya linaweza kuchochewa na aina ya virusi inayoambukizana sana ya B.1.1.7 na B.1.351 zilizogunduliwa mwezi Januari, kulingana na ripoti iliyotolewa na Africa CDC mnamo Machi 23.

Dkt. Kumantha pia alirejelea utafiti mpya kuhusu seli za T - aina ya seli nyeupe za damu - kuonyesha kwamba watu waliopona coronavirus walikuwa na seli za T ambazo zinaweza kutambuliwa kutoka nchini Uingereza, Brazil na Afrika Kusini.

"Kama janga la SARS-CoV-2 linavyoendelea, kuna uwezekano mkubwa kwamba aina mpya za virusi zitaibuka," unasema utafiti huo, uliochapishwa katika jarida la Open Forum Infectious Diseases, na Oxford University Press.