Makali ya corona: Watu 216 wapona corona, 18 waaga dunia, 137 waambukizwa corona

Muhtasari
  • Kenya imerekodi visa 137 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 1,641 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miaka 14 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 97
  • Jumla ya wagonjwa 1,265wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 6,614 wakiuguzwa nyumbani
Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Kenya imerekodi visa 137 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 1,641 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 160,559 kutoka kwa sampuli 1,681,420.

Katika visa hivi vipya, 129 ni raia wa Kenya huku 8 wakiwa raia wa kigeni, 80 ni wa kiume na 57 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miaka 14 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 97.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 216 wamepona virusi vya corona, 170 walipona wakiwa nyumbani huku 46 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 109,077 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 18 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 2,781 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,265wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 6,614 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 179 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).