Mchezaji wa raga Alex Olaba kurudi mahakamani

Muhtasari

Olaba alikamatwa Alhamisi wiki iliyopita, yeye na mchezaji mwenzake wa zamani Frank Wanyama wanakabiliwa na mashtaka ya ubakaji katika mahakama ya Milimani na wote wako nje kwa dhamana ya Shilingi 300,000.

Aliyekuwa mchezaji wa raga Alex Olaba
Aliyekuwa mchezaji wa raga Alex Olaba
Image: MAKTABA

Mchezaji wa raga Alex Olaba anafikishwa makamani hivi leo katika kesi mashtaka ya kujpanga kuua.

Olaba ambaye yuko nje kwa dhamana kutokana na kesi nyingine ya ubakaji anatarajiwa kujibu mashtaka ya kupanga njama kuua shahidi katika kesi ya ubakaji na kupanga njama ya kuvuruga haki.

Olaba alikamatwa Alhamisi wiki iliyopita, yeye na mchezaji mwenzake wa zamani Frank Wanyama wanakabiliwa na mashtaka ya ubakaji katika mahakama ya Milimani na wote wako nje kwa dhamana ya Shilingi 300,000.

Polisi walisema Olaba alikuwa akipanga kumuua shahidi muhimu katika kesi hiyo katika juhudi za kuvuruga upatikanaji wa haki.

Alikamatwa katika mtaa wa Nairobi West ambapo alikuwa akikutana na mpelelezi alikuwa akipanga mauaji ya shahidi huyo katika kesi ya ubakaji.

Polisi walisema walipata simu mbili kutoka kwa Olaba ambazo zinafanyiwa uchunguzi ili kubaini ikiwa kuna wahusika zaidi katika uhalifu huo.

Olaba alikuwa ameenda kwa mhusika mwingine akitafuta njia za kuondoa shahidi katika kesi hiyo na polisi wakaarifiwa.

Maafisa hao kisha walituma makachero ambao walijifanya kuwa tayari kumsaidia kushughulikia shahidi huyo kabla ya kesi yake kuanza tena.

Baada ya kukamatwa, Olaba aliwaambia polisi kwamba alikuwa amepagawa na roho za kishetani.

Olaba na Wanyama waliachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu ya Shilingi  300,000 na hakimu wa Mahakama ya Milimani Zainab Abdul baada ya kukana mashtaka ya ubakaji.

 Hii ilikuwa baada ya Mahakama Kuu kuagiza kusikilizwa upya kwa kesi dhidi ya wawili hao.

Mahakama kuu ilifutilia mbali hukumu yao na kifungo cha miaka 15 baada ya kusema kuwa hakukuwa na ushahidi kwamba mmoja wa mashahidi muhimu katika kesi hiyo aliapishwa kabla ya kutoa ushahidi.

Mwezi Agosti 2020, Hakimu Mkuu wa Milimani Martha Mutuku alikuwa ametoa uamuzi kwamba Wanyama na Olab

Aliyekuwa mchezaji wa raga Alex Olaba
Aliyekuwa mchezaji wa raga Alex Olaba
Image: MAKTABA