Covid-19:Watu 24 waaga dunia huku 345 wakipatikana na corona

Muhtasari
  • Watu 345 wamepatikana na corona siku ya Jumamosi Mei 1 kutoka kwa sampuli 6,686 zilizopimwa ndani ya saa 24

Watu 345 wamepatikana na corona siku ya Jumamosi Mei 1 kutoka kwa sampuli 6,686 zilizopimwa ndani ya saa 24.

Jumla ya idadi ya watu waliopatikana na corona imefika 160,904, huku jumla ya sampuli zilizopimwa nchini zikifika 1,688,106.

Kutoka kwa maambukizi hayo mapya 339 ni raia wa kenya ilhali 6 ni raia wa kigeni,195 ni wanaume ilhali 150 ni wanawake.

 

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miaka 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 94.

Nairobi inaongoza kwa visa 75 ikifuatwa na kaunti ya Uasin Gishu na visa 49.

Vile vile watu 140 wapona maradhi hayo,82 wamepona wakiwa nyumbani ilhali 58 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Jumla ya watu waliopona imefika 109,217

Kulingana na wizara ya afya watu 24 wamepoteza maisha yao kutokana na corona huku idadi ya jumla ya watu walioga dunia kutokana na corona ikifika 2,805.

Kifo 1 kimetokea katika masaa 24, wagonjwa 1,230 wamelazwa hospitalini, huku 6,654 wakipokea matibabu wakiwa nyumbani.

Pia kuna wagonjwa 154 katika kitengo cha wagonjwa mahututi, huku kufikia siku ya leo idadi ya waliopokea chanjo ikifika 894,076.