Rais Samia Suluhu Hassan awasili nchini Kenya

Muhtasari

Ndege iliyokuwa imembeba Rais Suluhu ilitua katika ardhi ya Kenya takriban dakika 15 kabla ya saa nne asubuhi, alikuwa ameabiri ndege ya shirika la Air Tanzania.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Image: HABARI MAELEZO TANZANIA

Rais Samia Suluhu Hassan amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimatiafa Jomo Kenya.

Hii ni ziara yake ya kwanza nchini Kenya tangu alipochukuwa mamlaka ya kuongoza taifa hilo kufuatia kifo cha aliyekuwa rais John Pombe Magufuli.

Ndege iliyokuwa imembeba Rais Suluhu ilitua katika ardhi ya Kenya takriban dakika 15 kabla ya saa nne asubuhi, alikuwa ameabiri ndege ya shirika la Air Tanzania.

Wananchi wametahadharishwa kuwa huenda msafara wake ukaathjiri shughuli za kawaida katika barabara kuu ya Mombasa - Nairobi akielekea katika ikulu ya rais.