Rais Suluhu: anakabiliana na dhana ya kutokuwepo kwa corona Tanzania

Muhtasari

• Ni chini ya miezi miwili tangu kifo cha rais John Pombe Magufuli aliyefariki akiwa na umri wa miaka 61, lakini makamu wake wa rais ambaye aliapishwa kuwa rais anaonekana kuchukua muelekeo tofauti.

Rais Samia akihudhuria ibada ya kumuaga Rais Magufuli
Rais Samia akihudhuria ibada ya kumuaga Rais Magufuli
Image: GETTY IMAGES

Mtangulizi wake alikuwa mzungumzaji lakini rais mpya wa Tanzania ni mtu mtulivu.

Pale ambapo mtangulizi wake amekuwa akichukua maamuzi ya pekee , mrithi wake amekuwa akijumuisha kila mtu.

Ni chini ya miezi miwili tangu kifo cha rais John Pombe Magufuli aliyefariki akiwa na umri wa miaka 61, lakini makamu wake wa rais ambaye aliapishwa kuwa rais anaonekana kuchukua muelekeo tofauti.

Ikija masuala ya covid 19, uhuru wa wanahabari ama kukabiliana na upinzani , amekuja na suluhu tofauti huku matamshi yake yakitolewa kwa njia ya utulivu lakini kwa ushawishi mkubwa.

Rais Samia aliapishwa siku mbili baada ya mtanguizi wake kufariki mwezi Machi
Rais Samia aliapishwa siku mbili baada ya mtanguizi wake kufariki mwezi Machi
Image: REUTERS

Hatahivyo , Rais huyo ameonekana kutopendelea kulinganishwa na Magufuli na amewashutumu wabunge wa Tanzania kwa kufanya hivyo

"Magufuli na Samia, ni watu wamoja . Nimekuwa nikifuatilia mjadala na nimesema sio mzuri kwa taifa letu , aliwaambia wabunge mwezi mmoja baada ya kuapishwa.

Lakini sio rahisi kutowalinganishakulingana na mwandishi na mchambuzi wa kisiasa Jesse Kwayu akisema kwamba kuna tofauti kubwa.

''Yeye ni mwenye busara na analeta ukali na umakini zaidi. Yeye ... anaelewa njia sahihi za mawasiliano na marekebisho."

Mara ya kwanza kabisa aliposimama jukwaani kama rais, muonekano wake, uchaguzi wake wa maneno na mwenendo uliahidi aina tofauti kabisa ya uongozi.

Ni uongozi ambao Tanzania haijawahi kuwa nao tangu Magufuli aliyepewa jina la 'Tingatinga' alipoingia madarakani 2015, hajali ambapo wengine wangebabaika, anafanya maamuzi ya busara'' alisema Deodatus Balile, Muhariri mkurugenzi wa kampuni ya habari ya Jamhuri Media Limited akimuelezea kuwa mwanadiplomasia.

"Anatambua kwamba Tanzania haiwezi kuishi ikiwa imejitenga na lazima tuwe ndani ya mfumo na kutazama masuala mengine pamoja na sehemu nyengine za ulimwengu.

Pengine tofauti yake kubwa ni jinsi anavyoliangazia janga la corona.

Chanjo na kufungwa kwa maeneo?

Magufuli alishutumu onyo liliotolewa na ulimwengu kuhusu virusi vya corona na kupuuza vitisho vyake akikataa kuruhusu chanjo ya corona nchini humo.

Wakati mmoja alitangaza kwamba virusi hivyo vimeshindwa na maombi nchini Tanzania.

Chini ya uongozi wa Magufuli raia wa Tanzania waliambiwa na mamlaka bila kutoa ushahidi kwamba kujifukiza kunasaidia kujilinda dhidi ya corona
Chini ya uongozi wa Magufuli raia wa Tanzania waliambiwa na mamlaka bila kutoa ushahidi kwamba kujifukiza kunasaidia kujilinda dhidi ya corona
Image: AFP

Hakuna takwimu za kuaminika kuhusu maambukizi au vifo kutokana na virusi ivyo Tanzania baada ya serikali ya magufuli kusita kutoa takiwmu hizo mwezi Mei mwaka uliopita.

Rais Samia kwa upande mwengine anatambua kwamba Tanzania haiwezi kupuuza virusi hivyo. Wiki tatu tu baada ya kuchukua madaraka , aliunda kamati ya wataalamu kuwashauri kuhusu hali ya virusi vya corona nchini na hatua muhimu zinazohitajika kuchukuliwa ili kuwaweka Watanzania salama.

Ameonekana akivalia barakoa , kitu ambacho Magufuli hakuwahi kufanya , ijapokuwa ni wakati alipokwenda Uganda na sio Tanzania.

Iwapo matamshi yake yanatoa tofauti kubwa kuhusu ugonjwa wa corona unavyochukuliwa na kubadili masuala kadhaa bado haijaonekana. Pia ni kweli kusema kwamba hakuna sera mpya imejitokeza kutoka kwa kamati hiyo ya wataalamu.

Huku kukiwa na mawimbi mapya ya ugonjwa huo ambayoi yanaripotiwa kila mahali duniani, wengi wako makini kujua tachukua hatua gani katika chanjo.

Watu pia wanasubiri kubaini iwapo huenda akachukua hatua ya kufunga baadhi ya maeneo ili kudhibiti ugonjwa huo hatua ambazo mtangulizi wake alikataa kuchukua.

Mikakati kama hiyo itaathiri mamilioni ya watu maskini Tanzania ikiwemo wafanyabiashara wadogowadogo ambao ndio msingi wa cha tawala cha mapinduzi CCM.

Iwapo atachukua mwelekeo huo , basi rais Samia atahitaji kuonesha uwezo wake wa ushawishi mkubwa kusema kwamba masharti hayo yatawasaidia wao wenyewe.

Lakini ana uwezo huo kulingana na bwana Kwayu.

Samia Suluhu ;alichaguliwa makamu wa rais pamoja na John Magufuli 2015.
Samia Suluhu ;alichaguliwa makamu wa rais pamoja na John Magufuli 2015.
Image: AFP

Maridhiano

Ameitaka wizara ya habari na utangazaji kubadili maamuzi yaliochukuliwa awali akisema serikali haipaswi kuwapatia raia fursa ya kusema kwamba serikali inakandamiza uhuru wa vyombo vya habari.

Rais pia amewasiliana na upinzani akiwa na lengo la kujadiliana jinsi watakavyoendesha masuala yao kwa faida za taifa.

Alikuwa na sifa za kuonesha maridhiano baada ya kumtembelea Kiongozi wa upinzani Tundu Lissu alipokuwa amelazwa hospitalini 2017 baada ya kupigwa risasi mara kadhaa na watu waliojihami katika jaribio la mauaji.

Alikuwa afisa wa serikali wa pekee kufanya hivyo.

Pia inatarajiwa kwamba rais Samia hatochukua misimamo mikali Zaidi ya ile ya Magufuli dhidi ya makampuni ya kimataifa nchini humo.

Mwaka 2017, Kampuni ya Accasia Mining ikiwa ni kampuni inayomilikiwa na kampuni ya Canada ya Barrick Gold ilipigwa faini ya kulipa kodi ya $190bn (£145bn) iliodaiwa na serikali ya Tanzania licha ya kwamba ilikana kufanya makosa yoyote .

Barrick ilifanikiwa kupunguza fedha hizo ikiwa ni mpango wake wa kupunguza deni hilo ambapo ni pamoja na kugawana faida za kiuchumi za siku zijazo na serikali kwa usawa.

Magufuli pia aliweka masharti mengi kwa biashara za kieneo kuingia soko la Tanzania na kuongeza masharti kwa bidhaa ambazo hazijasindikwa hususan kutoka Kenya Kuingia katika soko la taifa hilo.

''Matamshi yake hivi sasa ni kuhusu kukuza uwekezaji , kuimarisha biashara na kupanua ukusanyaji wa kodi'' , alisema Sanjay Rughani , ambaye anaongoza jopo la maafisa wakuu watendaji.

Kwa upande wa sekta ya ubinafsi , tunataka atuhusishe zaidi katika michakato ya serikali ilio na malengo ya kujenga Tanzania.

Rais Samia anatarajiwa kuwasili nchini Kenya siku ya Jumanne wiki sita tu baada ya kuapishwa , hatua hiyo ikilinganishwa na ziara 10 za Magufuli katika uongozi wake wa miaka sita, bwana Kwayu anasema kwamba anatumai kwamba rais mpya atakuwa na jicho la kimataifa.

''Nina hakika Tanzania itarejeshwa katika ramani ya Kimataifa, alisema. Itashiriki katika majadiliano ya kieneo kuhusu suluhu za mizozo na itawakilishwa katika maeneo kama vile Mikutano ya Umoja wa Mataifa''.

Kwake, yeye hatua tofauti aliyochukua rais Samia kuliongoza taifa hilo sio kumharibia jina mtangaulizi wake na badala yake kuchagua demokrasia na kufanya kile ambacho kilikuwa hakifanywi.

Bado ni lazima atembee katika njia ambayo inashirikisha serikali iliopita ambayo alikuwa ndani yake na mbinu mpya ya usimamizi ambayo inakubalika na maono ya wengi.