Vera sidika asema alikuwa bikira

Muhtasari

• Mwana sosholaiti Vera Sidika amesema  mchumba wake wa sasa, Mauzo alimpata akiwa embe bichi hajaonjwa na ndege yeyote mtini, bikra.

Vera Sidika
Vera Sidika

Mwana sosholaiti Vera Sidika amesema kamwe hamjui ‘Otile Brown’, Asema kuwa mchumba wake wa sasa, Mauzo alimpata akiwa embe bichi hajaonjwa na ndege yeyote mtini, akiwa bado bikra.

Mwanamitindo na mjasiriamali mwenye umbo la kuvutia Sidika amemkana aliyekuwa mpenzi wake mwanamziki anayetamba na kuteka anga Otile Brown.

Malkia huyu wa mitindo aliyejtosa ulingoni mwakai  2012 kutokana na video ya wimbo wa P-unit  ‘You Guy’ alikanusha kuwahi kuwa  na uhusiano au kumjua mwanamziki yule., kwenye ukurusa wake  wa Instagram alipoulizwa na shabiki mmoja kwenye kipindi cha maswali na majibu almaruufu kama Q&A.

“Naam, kwa kweli simjui OB ni nini ama ni nani. Nina hisia kwa bwanangu pekee” Vera alimjibu shabiki baada ya kumuuliza kama bado anazo hisia za mapenzi kwake Brown.

Vera Sidika na mpenzi wake wa sasa Brown Mauzo
Vera Sidika na mpenzi wake wa sasa Brown Mauzo

Wawili hao  walijitosa kwenye bahari ya huba na kuogelea kwa kipindi kifupi mwaka wa 2018 kisha wakaachana kutokana kile walitaja kama mzozo wa kifedha.

Kwa sasa Vera anaogelea kwenye bahari ya huba na mwanamziki mwingine aliyekita kambi mjini Brown Mauzo. Wawili hao walianza uhusiano mwaka uliopita huku madai yakienea mitandaoni kwamba wanapanga kufunga ndoa rasmi.

Vera pia alishangaza wengi kwenye kipindi hicho baada ya kudai kuwa Bwana Mauzo alimpata kama bado yeye ni bikra.

Otile Brown
Otile Brown

“Ikiwa kwa kusema  ‘virgo’ wamaanisha bikra, basi kweli alinipata nikiwa bikra” Vee alimjibu yule shabiki.

Madai haya yalizua gumzo moto mtandaoni mashabiki wakiuliza ikawaje yule binti aliyekuwa kwenye mahusiano yasiyopungua manne yanayojulikana bado akawa hajashiriki tendo la ndoa.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO