MAUAJI KWA FAMILIA

Msichana,15, aripotiwa kuuawa na wazazi na kaka yake

Baba, mama na kaka ya mwanafunzi wa Kiteta Girls wameshukiwa kumpiga msichana huyo wa miaka 15 hadi akakata roho baada yake kudaiwa kutoroka nyumbani na kutofika shule

Muhtasari

•Marehemu alikuwa mwanafunzi katika shule ya upili ya Kiteta Girls

•Muuguzi amethibitisha kuwa marehemu alikuwa na alama mwilini isharaa kuwa alishambuliwa vibaya

151
151

Baba, mama na kaka ya msichana mmoja wa miaka kumi na mitano  wamekamatwa na kufungiwa katika kituo cha polisi cha Kilimani kwa madai ya kumpiga msichana huyo hadi kufa.

Inadaiwa kuwa watatu, Frankline Ntwiga Marangu(baba), Benedetta Mbeni Muthoka(mama) na Ian Marangu(kaka, mwanafunzi wa TUK) walishirikiana kumpiga msichana huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Kiteta Girls baada ya kudaiwa kutoroka nyumbani na kukosa kufika shuleni.

Wapelelezi toka upande wa Kilimani wameanza uchunguzi kubaini uhakika wa kesi hiyo.

Hospitali ya Coptic kupitia mhudumu kwa jina Norine Mwende imearifu wapelelezi kuwa mnamo siku ya Alhamisi mida ya saa tatu usiku walimpokea msichana huyo aliyekuwa ameletwa na babake ili kupimwa kwani ilidaiwa alikuwa ametoroka nyumbani.

Baada ya kufanyiwa vipimo, msichana huyo alipewa ruhusa kuenda nyumbani ila marehem alirudishwa tena kwa dharura asubuhi ya kuamkia Ijumaa baada ya kuzirai akiwa nyumbani kutokana na kichapo alichopokea toka kwa baba, mama na kaka yake.

Inadaiwa kuwa alikuwa amekata roho wakati alifikishwa hospitali. Mhudumu katika hospitali hiyo ya Coptic alisema kuwa mwili wa marehemu ulikuwa umejaa alama ishara kuwa alikuwa ameshambuliwa vibaya.

Wapelelezi walipata mfereji aina ya PPR unaodaiwa kutumika katika kichapo hicho na kuubeba ili kutumika kama onyesho wakati kesi hiyo itakuwa inaendelea kotini.