•Mtapeli amekuwa akitumia kurasa za Instagram kama vile 'Bakcell Apple Store' na 'Netsol Apple store' kuwatapeli watu.
• Alikamatwa baada ya watu wengi waliokuwa wameanguka kwenye mtego wake kufikisha malalamishi kwa maafisa wa usalama
Mwanaume mmoja aliyeshukiwa kuwatapeli Wakenya kupitia mtandao wa Instagram alikamatwa na kuzuiliwa siku ya Jumanne.
Inadaiwa kuwa Victor Maina almaarufu kama 'Badman Anchor' amekuwa akitumia kurasa za Instagram kama vile 'Bakcell Apple Store' na 'Netsol Apple store' kuwaibia watu pesa huku akijifanya muuzaji mkubwa wa simu aina za iPhone na bidhaa zingine za kampuni ya Apple.
Maina alikamatwa baada ya watu wengi waliokuwa wameanguka kwenye mtego wake kufikisha malalamishi kwa maafisa wa usalama. Inadaiwa kuwa mtapeli huyo alikuwa ameibia watu kadhaa malaki ya pesa.
A man who has been defrauding unsuspecting members of the public, by posing as a dealer in high-end mobile phones and associated products, has this afternoon been arrested. pic.twitter.com/SBTKTsnJVa
— DCI KENYA (@DCI_Kenya) May 25, 2021
Mshukiwa huyo atafikishwa mahakamani kesho huku akishtakiwa kwa kosa la kupokea pesa kwa kutumia njia ya uwongo.