MAUAJI YA JENNIFER WAMBUA

Mshukiwa katika mauaji ya afisa wa NLC hayuko sawa

Sankala atafanyiwa uchunguzi zaidi kwa mara ya pili kutathmini hali yake tarehe 14 Julai baada ya uchunguzi wa kwanza kuonyesha kuwa hayuko sawa kiakili.

Muhtasari

•Sankala atafanyiwa tena uchunguzi zaidi wa kutathmini hali yake tarehe 14 Julai baada ya uchunguzi wa kwanza kuonyesha kuwa hayuko  sawa kiakili

•Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 22 Juni.

peter njenga
peter njenga
Image: George Owiti

Mshukiwa katika mauaji ya Jennifer Wambua ambaye alikuwa afisa wa tume ya ardhi(NLC) amekosa kujibu mashtaka huku ikisemekana kuwa hayuko sawa kiakili.

Mwendesha mashtaka wa taifa amesema kuwa Peter Njenga almaarufu kama Sankala hayuko timamu  kujisimamia mahakamani.

Wakili wa mshukiwa ,Dorine Mwau, aliambia koti kuwa Sankala alikuwa aende kufanyiwa uchunguzi zaidi wa kutathmini hali yake ya kiakili kwa mara ya pili tarehe 14 mwezi wa Julai baada ya uchunguzi wa kwanza kuonyesha kuwa mshukiwa hakuwa sawa kabisa kiakili.

Kesi hiyo iliskizwa katika mahakama kuu ya Machakos na jaji David Kemei.

Kemei aliamuru mshukiwa kurejeshwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga na kesi hiyo kutajwa tena tarehe 22 Juni.

Jennifer aliripotiwa kutoweka baada ya mumuwe kumsindikiza ofisini mwake mwezi wa Machi na baada ya sakasaka  mwili wake ukapatikana umetupwa katika msitu wa Ngong.