Covid-19:Watu 341 wapatikana na corona,144 wapona,11 waaga dunia

Muhtasari
  • Kenya imerekodi visa 341 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 3,646 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 169,697 kutoka kwa sampuli 1,796,585

Kenya imerekodi visa 341vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 3,646 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 169,697 kutoka kwa sampuli 1,796,585.

Katika visa hivi vipya, 329 ni raia wa Kenya huku 12 wakiwa raia wa kigeni, 174 ni wa kiume na 167 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 101.

Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 9.4%.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 144 wamepona virusi vya corona,96 walipona wakiwa nyumbani huku 48 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 115,988 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 11 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,108 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,067 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,680 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 104 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).