Covid-19:Watu 344 wapatikana na corona huku 16 wakipoteza maisha yao

Muhtasari
  • Kenya siku ya Ijumaa  imerekodi visa 344 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 4,864
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 170,041 kutoka kwa sampuli 1,801,449

Kenya siku ya Ijumaa  imerekodi visa 344 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 4,864 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 170,041 kutoka kwa sampuli 1,801,449.

Katika visa hivi vipya, 334 ni raia wa Kenya huku 10 wakiwa raia wa kigeni, 198 ni wa kiume na 146 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 93.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 30  wamepona virusi vya corona,3 walipona wakiwa nyumbani huku 27 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 116,018 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 16 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,124 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,188 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,712 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 107 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).