Covid-19:Watu 17 waaga dunia huku 444 wakipatikana na corona

Muhtasari
  • Watu 17 waaga dunia huku 444 wakipatikana na corona

Kenya siku ya Ijumaa imerekodi visa 444 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 4,989 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 170,485 kutoka kwa sampuli 1,806,438.

Katika visa hivi vipya, 435 ni raia wa Kenya huku 9 wakiwa raia wa kigeni, 259 ni wa kiume na 185 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 101.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 115 wamepona virusi vya corona,76 walipona wakiwa nyumbani huku 39 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 116,133 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 17 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,141 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,171 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,682 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 104 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).