Covid-19:Watu 643 wapona corona,16 waaga dunia huku 162 wakipatikana na corona

Muhtasari
  • Watu 162 wapatikana na virusi vya corona, hii ni kutoka kwa sampuli 3,452 zilizopimwa chini ya saa 24
  • Idadi JUmla ya watu walioambukizwa virusi vya corona imefika 170,647, huku idadi ya sampuli zilizopimwa ikifika 1,809,890

Watu 162 wapatikana na virusi vya corona, hii ni kutoka kwa sampuli 3,452 zilizopimwa chini ya saa 24.

Idadi JUmla ya watu walioambukizwa virusi vya corona imefika 170,647, huku idadi ya sampuli zilizopimwa ikifika 1,809,890.

Kati ya maambukizi hayo ya jumapili 152 ni raia wa kenya ilhai 10 ni raia wa kigeni, wagonjwa 116 ni wakiume ilhali 46 ni wa kike.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miaka 17 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 70.

Kaunti ya Nairobi imeongoza kwa visa 55, huku ifuatwa na kaunti ya Busia kwa busia 32, alafu kaunti ya Homabay,Mombasa na Kilifi visa 10 mtawalia.

Kulingana na wizara ya afya watu 643 wamepona maradhi ya corona, 406 wamepona huku wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 237 wakiruhusiwa kuenda nyumbani.

Idadi jumla ya watu waliopona imefika 116,776.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 16 wameaga dunia kutokana na corona, idadi ya walioaga dunia kwa sasa imefika 3,157.

Wagonjwa 1,225 wamelazwa hospitalini huku 4,724 wakijitenga nyumbani, kuna wagonjwa 93 katika kitengo cha wagonjwa mahututi.