Mwanamume azuiliwa na polisi akikimbia kuelekea kwa rais na kukatiza hotuba

Muhtasari
  • Mwanamume azuiliwa na polisi akikimbia kuelekea kwa rais na kukatiza hotuba
  • Sherehe hizo zilifanyika katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Kisumu

Mwanamume Jumanne alizuiliwa na polisi wakati akikimbia kuelekea kwa Rais Uhuru Kenyatta alipokuwa anatoa hotuba yake wakati wa sherehe ya Siku ya Madaraka ya 58.

Sherehe hizo zilifanyika katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Kisumu.

Mwanamume huyo aliibuka kutoka kwa umati wakati Uhuru alikuwa akitoa hotuba yake na kukimbilia uwanjani, na kukatisha sherehe hiyo, lakini maafisa wa usalama walichukua hatua haraka na kumpeleka mbali na uwanja huo.

Ilibidi Uhuru asimamishe hotuba yake na kuwaambia maafisa wamwachie mtu huyo.

"Acheni aende, kwa biashara zake, tunaweza endelea sasa," Rais alisema huku akitabasamu.

Baada ya onyesho la hewani mbele ya Uhuru na waheshimiwa wengine, waendesha parachut walionyesha umahiri wao walipokuwa wakitua uwanjani.

Walakini, mmoja wao alitua vibaya na kulazimisha jibu la haraka na wahudumu ambao walimpakia kwenye gari la wagonjwa lililokuwa likingojea.