Covid-19: watu 18 waaga dunia,16 wapona,142 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Kenya  imerekodi visa 142 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 2,650 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 171,226 kutoka kwa sampuli 1,818,416

Kenya  imerekodi visa 142 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 2,650 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 171,226 kutoka kwa sampuli 1,818,416.

Katika visa hivi vipya, 131 ni raia wa Kenya huku 11 wakiwa raia wa kigeni, 76 ni wa kiume na 66 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miaka 14 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 83.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 16 wamepona virusi vya corona,7 walipona wakiwa nyumbani huku 9 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 117,039 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 18 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,206 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,251 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,705 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 92 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).