Covid-19:Idadi ya corona imefika 171,658 baada ya watu 432 kupatikana na corona

Muhtasari
  • Watu 17 waaga dunia kutokana na corona, huku 306 wakipona maradhi hayo

Kenya imerekodi visa 432 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 3,800 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 171,658 kutoka kwa sampuli 1,822,216

Katika visa hivi vipya, 424ni raia wa Kenya huku 8 wakiwa raia wa kigeni, 229 ni wa kiume na 203 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 4 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 91.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 306 wamepona virusi vya corona,217 walipona wakiwa nyumbani huku 89 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 117,345 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 17 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,223 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,227 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,957wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 102 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).