Covid-19:Watu 624 wapatikana na corona,17 waaga dunia

Muhtasari
  • Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 4 ilhali mwenye umri wa juu ana miaka 94
Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Visa 624  vipya vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini siku ya JUmatano kutoka kwa sampuli 6,724 na kufkisha idadi jumla ya 174,285  vya maambukizi ya maradhi hayo.

Kati ya visa hivyo vipya 567 ni wakenya ilhali 57 ni raia wa kigeni,405 ni wagonjwa wa kiume huku 219 wakiwa wa kike.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 4 ilhali mwenye umri wa juu ana miaka 94

Kulingana na wizara ya afya watu 313 wamepona maradhi hayo na kufikisha idadi jumla ya 119,246 ya watu waliopona corona.

258 wamepona wakipokea matibabu wakiwa nyumbani huku 55 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hopitali mbalimbali nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha ni kuwa watu 17 wameaga dunia kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 3,362 ya watu walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 991 ambao wamelazwa hospitalini, huku 4,940 wakipokea matibabu wakiwa nyumbani.

Vile vile wagonjwa 111 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).