Mwanafunzi amdunga mwalimu mkuu msumari kichwani Kericho

Muhtasari

• Mwanafunzi huyo anasemekana kugeuza ubao uliokuwa na msumari siku ya Jumatano, Juni 9, na kupigilia msumari ndani ya kichwa

crime scene
crime scene

Polisi  katika kaunti ya Kericho wameanzisha msako kutafuta mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Ainamoi huko Ainamoi baada ya kumshambulia mwalimu mkuu wa shule hiyo kwa kumdunga kichwani kwa msumari wa inchi nne.

Mwanafunzi huyo anasemekana kugeuza ubao uliokuwa na msumari siku ya Jumatano, Juni 9, na kupigilia msumari ndani ya kichwa cha mwalimu huyo, kulingana na Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Kericho Silas Gichunge.

Kulingana na rakaunti, shambulio hilo la umwagaji damu lilikuja baepoti za polisi mwalimu mkuu alikuwa amemuuliza mwanafunzi huyo kulipa salio lake la karo la  Ksh.7,000.

Polisi  wanasema mwalimu huyo mkuu alikuwa ameamuru dawati la mwanafunzi huyo lichukuliwe hadi deni lilipwe.

Siku moja baadaye, mwanafunzi huyo alimvizia mkuu wa shule wakati akitoka shuleni na kumpiga kwa ubao huo.

Wanafunzi walioshuhudia shambulio hilo walipiga kamza na kuvuta umati wa za watu waliokuwa wakimpeleka mwalimu hospitalini.