283 wapatikana na COVID 19; Vifo 9 vyaripotiwa

Wagonjwa 99 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi

Muhtasari

•Mtoto wa miaka miwili ndiye mgojwa mchanga zaidi wakati mgonjwa mzee zaidi akiwa na miaka 92.

•atu 995,012 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chano dhidi ya Korona kufikia leo. Hata hivyo, 188,364 pekee kati yao ndio wamepokea dozi zote mbili.

Watu 283 wamepatikana na virusi vya Korona kati ya 3, 452 waliopimwa ndani ya kipindi cha masaa ishirini na manne yaliyopita.  Hii inaashiria kuwa asilimia ya maambukizi inasimamia 8.2%. 

Wanawake waliopatina na virusi hivyo ni 151 ilhali wanaume ni 132. 272 kati ya wagonjwa hao  ni Wakenya ilhali 11 ni wageni. `

Mtoto wa miaka miwili ndiye mgojwa mchanga zaidi wakati mgonjwa mzee zaidi akiwa na miaka 92.

Jumla ya vipimo 1,904,519 vimefianya Kufikia leo na, watu 179,075 wamepatikana na ugonjwa wa COVID 19 kwa wakati mmoja au mwingine .

Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa maambukizi ikiandikisha wagonjwa 88 huku ikifuatiwa na Kisii, Kisumu, Mombasa, Siaya, Homabay, Busia, Nandi ambazo zimeandikisha wagonjwa 33, 26, 24, 19, 15, 10, 10 na 10 mtawalia.

 Zingine ni Meru 7, Kilifi 7, Kakamega 6, Nakuru 5, Narok 3 huku Kiambu, Kwale, Machakos, Taita Taveta na Bungoma zikiandikisha wagonjwa wawili kila mmoja.

Muranga, Nyamira, Nyeri, Bomet, Lamu, Turkana, Vihiga, Elgeyo Marakwet, Isiolo, Kajiado na Kericho ziliandikisha mgonjwa mmoja mmoja.

Wagonjwa 73 waliweza kupona ndani ya kipindi cha masaa 24 huku 61 wakiponea nyumbani na 12 kutoka vituo mbalimbali vya afya.

Habari ya kusitikisha ni kuwa vifo 9 kutokana na maradhi ya COVID 19 vimerekodiwa kutoka vituo mbali mbali nchini. Hii inapelekea idadi ya wafu kutokana na Corona kuwa 3,456.

Jumla ya wagonjwa 1106 wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali mbali mbali  huku wagonjwa 5,488 wakiendelea kuhudumiwa manyumbani.

Wagonjwa 99 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi

Watu 995,012 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chano dhidi ya Korona kufikia leo. Hata hivyo, 188,364 pekee kati yao ndio wamepokea dozi zote mbili.