Makali ya corona:Watu 30 waaga dunia kutokana na corona

Muhtasari
  • Watu 622 wapatikana na corona,30 waaga dunia
  • Pia mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 93
  • Watu 313 wamepona corona na kufikisha idadi jumla ya 123,363 ya watu waliopona maradhi ya corona

Kenya siku ya Jumatano imerekodi visa 622 vipya vya maambukizi ya corona, kutoka kwa sampuli 6,236zilizopimwa ndani ya saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya maambukizi ya corona imefika 180,498  huku jumla idadi ya sampuli ikifika 1,920,018.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 590 ni wakenya ilhali 32 ni raia wa kigeni, vile vile 369 ni wanaume ilhali 253 ni wa kike.

Pia mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 93.

Watu 313 wamepona corona na kufikisha idadi jumla ya 123,363 ya watu waliopona maradhi ya corona.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 30 wamepoteza maisha yao kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 3,514ya watu walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 1,053 ambao wamelazwa hospitali huku 6,612  wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani.

Wagonjwa 101 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi,