Rais wa zamani Jacob Zuma kufungwa gerezani

Muhtasari

• Zuma aliptikana na hatia ya kupuuza agizo la kufika mahakamni kujibu kesi ya ufisadi iliyokuwa ikimkabili.

zuma in court
zuma in court

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepatikana na hatia ya kukaidi maagizo ya mahakama.

Zuma ambaye alifurushwa mamlakani na chama chake ca ANC kabla ya muhula wake kukamilika alipatikana na hatia ya kupuuza agizo la kufika mahakamni kujibu kesi ya ufisadi iliyokuwa ikimkabili.

Mahakama nchini Afrika Kusini iliamua kuwa rais huyo wa zamanai afungwe kifungo cha miezi 15 gerezani kwa kosa hilo. 

Mahakama ilikuwa na jukumu la kuamua kama Zuma alifaa kuadhibiwa kwa kukataa wito wa mahakama na amri ya mahakama ya kumtaka afike mahakamani kutoa ushahidi kuhusu shutuma za rushwa wakati wa utawala wake.

Mwenyekiti wa kamati maalum ya uchunguzi wa mahakama, Raymond Zondo ambayo imekuwa ikichunguza madai hayo aliiomba mahakama itamke kuwa rais huyo wa zamani alidharau mahakama na imhukumu kifungo cha miaka miwili.

Tangu alipojiuzulu mnamo mwaka 2018, Bwana Zuma amekuwa akifika mahakamani akikabiliwa na shutuma za ufisadi ambazo amekuwa akizikanusha.