531 wapatikana na COVID 19, Vifo 20 vyaripotiwa

Wagonjwa 124 wa COVID 19 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Muhtasari

•Mtoto wa mwaka mmoja na mkongwe wa miaka 93 ni miongoni mwa  waliopimwa na kupatikana na virusi hivyo.

•Wagonjwa 1144 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya nchini huku wagonjwa 5,785 wakiendelea kuhudumiwa manyumbani.

 

Virusi vya Korona
Virusi vya Korona
Image: Hisani

Watu 531 wamepatikana kuwa na virusi vya Corona kati ya 8,154 waliopimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

16 kati yao ni raia wa kigeni ilhali wengine 515 wote ni Wakenya. Kwa sasa asilimia ya maambukizi ni 6.5%.

Mtoto wa mwaka mmoja na mkongwe wa miaka 93 ni miongoni mwa  waliopimwa na kupatikana na virusi hivyo.

Kwa upande mwingine, watu 276 waliweza kupona huku 151 kati yao wakiponea manyumbani ilhali 125 walipata nafuu wakiwa wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya.

Hata hivyo, Kenya imerekodi vifo 20 vyote vikiwa ripoti ya kuchelewa kutoka vituo mbali mbali vya afya.

Kufikia sasa, watu 185, 591 wamekuwa waathiriwa wa COVID 19 kati ya 1,978, 155 ambao wamepimwa tangu ujio wa janga la Corona. Watu 3,671 wamepoteza maisha yao kutokana na ugonjwa huo kufikia leo.

Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa maambukizi baada ya kurekodi wagonjwa 185. Uasin Gishu inafuata na 43 kisha Busia n 38.

Kiambu ilirekodi visa 30, Siaya 28, Kilifi 28, Nakuru 28, Kisumu 24, Migori 20, Kakamega 14, Nyamira 12,  Kericho 12, Homa Bay 9, Kajiado 6, Laikipia 5, Kisii 4, Kwale 4, Taita Taveta 4, Nyandarua 4, Murang'a 4. Baringo, Kitui,Machakos, Meru na Turkana ziliandikisha wagonjwa watatu kila mmoja.

Bungoma na Bomet ziliandikisha wagonjwa wawili wawili ilhali Kirinyaga, Mombasa, Narok, Nyeri na West Pokot zilirekodi mgonjwa mmoja mmoja

Wagonjwa 1144 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya nchini huku wagonjwa 5,785 wakiendelea kuhudumiwa manyumbani.

Wagonjwa 124 wa COVID 19 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo dhidi ya COVID 19

Kufikia leo, watu 1,016, 190 wamepokea chanjo ya kuzuia virusi vya Corona nchini huku 452, 718 kati yao wakipokea chanjo zote mbili.