Naibu rais akutana na wajumbe 227 kutoka eneo la mlima Kenya

Ruto anatarajiwa kuzindua mpango wake wa uchumi mwezi Desemba.

Muhtasari

•Naibu rais William Ruto alikutana na madiwani 227 wa eneo la mlima Kenya siku ya Jumamosi  kwake  mjini Karen.

•Mkutano na madiwani  wa mlima Kenya unakuja wiki mbili tu baada ya mkutano kama huo kufanyika na madiwani wa kutoka kaunti ya Baringo.

William Ruto
William Ruto
Image: Hisani

Habari na Gideon Keter

Naibu rais William Ruto alikutana na madiwani 227 wa eneo la mlima Kenya siku ya Jumamosi  kwake  mjini Karen.

Madiwani hao waliongeleshwa kuhusu manifesto ya UDA na mfumo wa uchumi wa kutoka chini kwenda juu. Ruto anatarajiwa kuzindua mpango wake wa uchumi mwezi Desemba.

Mkutano na madiwani  wa mlima Kenya unakuja wiki mbili tu baada ya mkutano kama huo kufanyika na madiwani wa kutoka kaunti ya Baringo.

Mwezi uliopita, mrengo unaojihusisha na rais Uhuru Kenyatta ulipoteza wafuasi kadhaa kutoka eneo la kati la Kenya ambao walijiunga na mrengo wa 'Hustler'. Kuhama huko  kunaonekana kama njia ya kuimarisha noa ya naibu rais kutwaa kitu cha urais mwaka ujao.

Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kiambu Gathoni wa Muchomba, mbunge wa Nakuru Mashariki David Gikaria na yule wa Githunguri Gabriel Kago walijiunga na mrengo wa naibu rais