Watu 669 wapona COVID 19; 1126 wamelazwa hospitalini

Kufikia sasa watu 1,017,485 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya COVID 19 huku 456,384 wakiweza kupokea dozi zote mbili.

Muhtasari

•Mtoto wa miezi 10 ni miongoni mwao huku mkongwe wa miaka 95 akiwa mtu mzee zaidi kwenye idadi hiyo.

•Wagonjwa 115 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe

Kenya imerekodi wagonjwa 277 wa ugonjwa wa COVID 19 kati ya 3,796 ambao wamepimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

Hii inaashiria kuwa asilimia ya maambukizi kwa sasa imesimamia 7.3%.

5 kati ya waliopatikana na virusi vya Corona ni raia wa kigeni ilhali wengine wote 272 ni Wakenya.

Mtoto wa miezi 10 ni miongoni mwao huku mkongwe wa miaka 95 akiwa mtu mzee zaidi kwenye idadi hiyo.

Kufikia sasa watu 185,868 kati ya 1,981,951 waliopimwa ndio waliowahi kupatikana na virusi vya Corona.

Kaunti ya Nairobi imeendelea kuongoza kwa maambukizi ikirekodi visa 64 ikifuatiwa na Mombasa 31, Nandi 27, Siaya 22, Busia 17, Uasin Gishu 16, Homabay 10, Kericho 9, Kisumu 9, Bungoma 7, Narok 7, Embu 6.

Kilifi na Migori ziliandikisha wagonjwa 5 kila mmoja ilhali Kakamega, Lamu na Kiambu zilirekodi wagonjwa 4. Bomet, Meru na Taita Taveta wagonjwa 2 huku Kitui na Murang'a zikiandikisha mgonjwa mmoja mmoja.

Wagonjwa 669 waliweza kupona kwenye kipindi cha masaa 24 yaliyopita , 588 wakiponea nyumbani ilhali 81 waliponea hospitalini. Vifo vinne vilirekodiwa.

Wagonjwa 1,126 ndio wamelazwa katika vituo mbalimbali vya afya huku 5,834 wakiendelea kuhudumiwa nyumbani. 

Wagonjwa 115 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo

Kufikia sasa watu 1,017,485 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya COVID 19 huku 456,384 wakiweza kupokea dozi zote mbili.