logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Covid-19: Watu 1,186 wapona corona,15 Waaga dunia

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 186,053 kutoka kwa sampuli 1,983,998.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri05 July 2021 - 13:15

Muhtasari


  • Kenya imerekodi visa 185 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 2,047 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 186,053 kutoka kwa sampuli 1,983,998
  • Katika visa hivi vipya, 171 ni raia wa Kenya huku 14 akiwa raia wa kigeni, 112 ni wa kiume na 73 ni wanawake

Kenya imerekodi visa 185 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 2,047 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 186,053 kutoka kwa sampuli 1,983,998.

Katika visa hivi vipya, 171 ni raia wa Kenya huku 14 akiwa raia wa kigeni, 112 ni wa kiume na 73 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miaka 5 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 91.

Kulingana na wizara ya afya kaunti ya Nairobi imeongozwa kwa visa  94, Bungoma 25,Mombasa 16, Machakos 11, Kakamega 7, Tana River 5, Kilifi 5, mtawalia.

Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 9.0%.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 1,186 wamepona virusi vya corona,1,102 walipona wakiwa nyumbani huku 84 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 128,811 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 15 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,690 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,151 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 5,426 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 119 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved