Makali ya corona:Asilimia ya maambukizi nchini ni 7.9%, 7 waaga dunia

Muhtasari
  • Watu 400 wamepatwa na maambukizi ya corona kutoka kwa sampuli 5,068 zilizopimwa ndani ya saa 24
Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Watu 400 wamepatwa na maambukizi ya corona kutoka kwa sampuli 5,068 zilizopimwa ndani ya saa 24.

Kutoka maambukizi hayo mapya 220 ni wanaume huku 180 wakiwa ni wagonjwa wa kike, pia 386 ni wakenya 14 ni raia wa kigeni.

Asilimia ya maambukizi nchini leo ni 7.9%, jumla idadi ya maambukizi nchini imefika 186,453 kutoka kwa idadi jumla ya sampuli 1,989,066.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana siku 12 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 97.

Watu 354 wamepona maradhi ya corona, 259 wamepona wakiwa nyumbani ilhali 95 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka kwa hospitali tofauti.

Idadi jumla ya watu waliopona kutoka kwa corona imefika 129,165.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 7 wameaga dunia kutokana na corona, idadi jumla ya watu walioaga dunia kutokana na corona imefika 3,697.

Kuna wagonjwa 1,133 ambao wamelazwa hospitali huku 5,387 wakipokea matibabu wakiwa nyumbani.

Wagonjwa 113 wako katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).