logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mbunge Babu Owino afanya jaribio jingine la kutatua kesi yake na DJ Evolve nje ya mahakama

Mwendesha mashtaka alithibitisha kwamba kweli mazungumzo yameendelea

image
na Radio Jambo

Habari07 July 2021 - 12:31

Muhtasari


  • Familia ya DJ Evolve na Babu Owino kukamilisha mazungumzo ili kesi kusuluhusihwa nje ya korti
Babu Owino

HABARI NA ANNETTE WAMBULWA;

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amefanya jaribio jingine la kutatua kesi yake na DJ Evolve  nje ya mahakama.

Mbunge alishtakiwa kwa kujaribu kuua Evolve ambaye alipiga risasi kwenye klabu moja  huko Kilimani.

Mwanasheria wa familia ya DJ Evolve ameiambia mahakama kuwa wako katika hatua za mwisho za mazungumzo.

Mhakimu Mkuu  Bernard Ochoi alisikia kwamba jambo pekee ambalo linalowazuia ni nyaraka ambazo wanapaswa kuwasilisha kwa mashtaka.

Mwendesha mashtaka alithibitisha kwamba kweli mazungumzo yameendelea kati ya mshtaki na mshtakiwa.

Mahakama hiyo pia ilisikia kwamba mashtaka yalifanya mikutano miwili kati ya Babu na Evolve pamoja na wanasheria wao.

"Wote tunasubiri hati kutoka kwa wawili hao ambayo itatuwezesha kutoa kwa DPP kwa maelekezo" Mwendesha mashtaka alisema.

Mwendesha mashtaka aliomba  muda zaidi akisema mwendesha mashtaka anayeshughulikia kesi hilo Nyamosi alikuwa mbali na wajibu rasmi na yeye ndiye anayetakiwa kupeleka barua kwa DPP.

Ochoi aliamua kwamba suala hilo litatajwa katika wiki tatu ili kuwawezesha muda zaidi wa kukamilisha mazungumzo.

Jaribio la kwanza la Babu la kutatua kesi hiyo nje ya mahakamaliligonga mwamba  baada ya Ochoi kukataa kuondoa kesi hiyo bila kuwa na taarifa nini Babu alichokuwa anampa DJ Evolve

Ochoi alisema angeweza kuondoa kesi hiyo kama pande zote mbili zingeweza kusuluhisha tatizo.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved