Makali ya corona:Watu 1,934 wapona corona,11 waaga dunia

Muhtasari
  • Kenya imerekodi visa 566 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 5,344 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 187,525 kutoka kwa sampuli 12,001,786
  • Katika visa hivi vipya, 546 ni raia wa Kenya huku 20 akiwa raia wa kigeni, 318 ni wa kiume na 248 ni wanawake

Kenya imerekodi visa 566 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 5,344 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 187,525 kutoka kwa sampuli 12,001,786.

Katika visa hivi vipya, 546 ni raia wa Kenya huku 20 akiwa raia wa kigeni, 318 ni wa kiume na 248 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 11 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 97.

Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 10.6%.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 1,934 wamepona virusi vya corona,1,693 walipona wakiwa nyumbani huku 241 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 176,456 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 11 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,716 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,136 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,825 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 116 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU