Kenya inahitaji uongozi!Wabunge wa ANC wasema hamna haja ya kufufua NASA

Muhtasari
  • Wabunge wa ANC wasema hamna haja ya kufufua NASA
  • Wamesema kuwa Mudavadi raundi hii hatarudi nyuma na kuangalia mkondo wa mambo ndani ya NASA bali lengo ni kusaka marafaiki wapya

Viongozi wa chama cha ANC na wenzao wanaounga mkono azma ya urais ya kinara wa ANC Musalia Mudavadi wamepasua mbarika na kusema kuwa hawana Imani ya kufufuliwa kwa mrengo wa upinzani, NASA.

Viongozi hawa wakiongozwa na Seneta wa kaunti ya Kakamega Cleophas Malalah pamoja na wabunge Bishop Titus Khamala na Tindi Mwale wamesema kuwa ndoa ya NASA imekuwa na majaribu na masaibu mengi na sasa imekosa ladha.

Wakizungumza katika kanisa la Jesus Teaching Ministry eneo la Embakasi West kwenye ibaada ya jumapili walipokuwa wameandamana na Kinara wa ANC Musalia Mudavadi viongozi hao wanadai kuwa kutoaminiana ndani ya NASA ni Ishara tosha kuwa kufufua NASA kutasalia kuwa ndoto ya mizaituni.

“Kuna mtu alisema hataki Musalia na Kalonzo na wengine ati hawatamsaidia kwasababu ako na watu

Nataka nimwambie huyo mtu no politician owns Kenyans Kenyans belong to God usiseme watu ni wako

Sisi huyo mtu tunamuambia tunamuangalia Musalia Mudavadi kwa sababu ya chatacter yake. Hatutaki endorsments tutatafuta marafiki

Unajua Lutu kwa Bibilia walipokuwa wakiondoka baada ya kuamurishwa na Mungu mke wake aliangalia nyuma na akawa jiwe la chumvi. NASA ili NASWA and we are not looking back to NASA. Musalia angalia mbele twende mbele.” Titus Khamala.

Seneta Cleophas Malala akizungumza katika hafla hiyo alikuwa na haya ya kusema.

“Sisi Kama Chama cha ANC tumekuwa kwa abusive marriage kwa miaka 5. Bwana haleti chakula na kikipatikana kidogo anakula peke yake

Ikifakika mahali akaenda kwa mpango wa kando akatuacha. Sasa Apostle tuombee kwasababu umesema tuwe na vision ya kuenda mbele kuba shetani anajaribu kusema turudi nyuma kwa ndoa ya NASA, tunaomba sana Party Leader wetu asirudi huko

Musalia Mudavadi is the right person for this Country naskia kuna Hustler na wale wengine hawa watatugawanyisha kwa misingi ya kikabila Nusu ya Kenya itafurahia na Nusu ya Kenya itakasirika

Kwa hivyo maombi ya wakenya yule mti neutral ambaye atasaidia Kenya iwe kitu kimoja na isonge mbele hasa kukomboa uchumi na kuleta amani ni Musalia Mudavadi.” Cleophas Malalah alizungumza.

Viongozi hao wamemtaka Mudavadi kuwa na maono makuu ya kulikomboa taifa hili wakisema kuwa wakati umefika wa Kenya kupata kiongozi ambaye ataunganisha wakenya wote bila kuzingatia misingi ya kikabila wala mapato.

Wamesema kuwa Mudavadi raundi hii hatarudi nyuma na kuangalia mkondo wa mambo ndani ya NASA bali lengo ni kusaka marafaiki wapya na kubuni miungano mipya yenye ajenda ya kufufua uchumi, kutoa nafasi za ajira kwa wakenya na kuleta amani.

Viongozi wengine waliokuwepo wakisema kuwa Kenya kwa sasa inahitaji uongozi ambao ni thabiti na kudai kuwa Mudavadi ndiye chaguo bora. Msimamo huu ambao umeibuka baada ya semi kadhaa kuibuka kuwa kuna uwezekano wa kufufuliwa kwa muungano wa NASA ni ishara tosha kuwa huenda kila mwamba ngoma anavutia upande wake.

“What Kenyans want is leadership. Hii mambo ya watu kufanya hadi tunaagiza mahindi na mayai kutoka nje sio jambo mzuri. Madimoni ya 2013 imeisha sasa na Mudavadi ndiye kiongozi ambaye wakenya wanatazamia kwa sasa.” Marende alisema.

Mudavadi kwa upande wake ameshikilia kuwa kuna umuhimu wa taasisi ambazo zitasimamia uchaguzi hasa IEBC kuweka mikakati bora ili wakenya waweze kupewa nafasi ya kufanya maamuzi ya busara ifikiapo debe la mwaka 2022.

“Tuombe Kenya iwe na amani wakati wa mpito. Tusiende kwa Transition kisha watu waanze kumwaga damau. Wakenya waachwe wawachague viongozi wao bila kushurutishwa wala kutishwa tishwa.” Musalia Mudavadi.

Mudavadi akiwa aliendeleza msukumo wake wa sera zitakazoangazia kufufuliwa kwa uchumi amesema kuwa kuna haja ya wakenya kuwaweka kwenye mizani wale viongozi ambao watawatwika mammlaka na kusisitiza kuwa ajenda ya uchumi bora na pesa mfukoni ndio nguzo ambayo ANC itatumia kuwasaka waandani wapya wa kisiasa kukiwa tayari kuna mazungumzo kuhusu One Kenya Alliance huku NASA na ndoto zake ikionekana kuzidi Kunaswa.

“Agenda ya ANC itasalia kuwa Uchumi Uchumi Uchumi. Maisha ni Magumu n ani sharti tuangazie jinsi ya kuwakomboa wakenya.” 

Mudavadi akiwa wikendi hii alikita maeneo ya Eastlands Nairobi kwenye pita pita zake za kuzidi kuuza sera zake kama mmoja wa wagombeaji bora zaidi kumrithi Rais Uhuru Kenyatta ifikiapo mwaka 2022.