Makali ya corona:Watu 241 wapatikana na corona,1,401 wapona,1 aaga dunia

Muhtasari
  • Katika visa hivi vipya, 222 ni raia wa Kenya huku 19 akiwa raia wa kigeni,144 ni wa kiume na 97 ni wanawake
  •  
    Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 6 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 93
  • Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 8.1%

Watu 241 wamepatikana na maambukizi COVID-19 kutoka kwa sampuli 2,961 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 188,754  kutoka kwa sampuli 2,015,659.

Katika visa hivi vipya, 222 ni raia wa Kenya huku 19 akiwa raia wa kigeni,144 ni wa kiume na 97 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 6 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 93.

Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 8.1%.

Watu 1,401 wamepona virusi vya corona,1,380 walipona wakiwa nyumbani huku 21 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 179,520 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba Mtu 1 ameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,722  watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,092 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,077 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 115 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU