logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Makali ya corona: Watu 761 wapatikana na corona,71 wapona,9 waaga dunia

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 189,703 kutoka kwa sampuli 2,023,807.

image
na Radio Jambo

Burudani13 July 2021 - 14:05

Muhtasari


  • Kenya  siku ya Jumanne imerekodi visa 761 vipya vya maambukizi  ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 5,794 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 189,703 kutoka kwa sampuli 2,023,807
  • Katika visa hivi vipya, 727 ni raia wa Kenya huku 34 akiwa raia wa kigeni,381 ni wa kiume na  ni 380 wanawake

Kenya  siku ya Jumanne imerekodi visa 761 vipya vya maambukizi  ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 5,794 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 189,703 kutoka kwa sampuli 2,023,807.

Katika visa hivi vipya, 727 ni raia wa Kenya huku 34 akiwa raia wa kigeni,381 ni wa kiume na  ni 380 wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 6 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 96.

Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 13.0%.

Watu 71 wamepona virusi vya corona,45 walipona wakiwa nyumbani huku 26 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 180,624 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 9 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,732  watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,067 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,359 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 123 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved